×

Yanga Hakuna Kulala, Gamondi Amepania Balaa

KOCHA Mkuu wa Yanga, Muargentina, Miguel Gamondi, nguvu na hasira zake zote amezihamishia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara watakaocheza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Hiyo ni baada ya kutoka kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama ya nchini Ghana, katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao Yanga walikuwepo ugenini.

Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, Desema 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema kuwa wameuweka kando mchezo wao wa marudiano dhidi ya Medeama na sasa akili zao wanazielekeza mechi na Mtibwa Sugar ambao upo mbele yao.

Gamondi alisema kuwa anaamini kikubwa wanarejea katika ligi, kwa lengo moja pekee ambalo kushinda kila mchezo uliokuwepo mbele yao, kwa kuanza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Aliongeza kuwa, baada ya mchezo dhidi ya Medeama, alifanya kikao na wachezaji wake, kuwataka kusahau matokeo hayo ya sare tya bao 1-1 waliyoyapata na badala yake waelekeze akili na nguvu zao katika ligi watakapocheza na Mtibwa.

“Kila mchezo tunauchukulia umuhimu mkubwa, na kikubwa ni kupata ushindi na siyo kkitu kingine, ninaheshimu kila mpinzani nitakayekutana naye mbele katika ligi na mashindano ya kimataifa.

“Wachezaji nimewaambia wasahau matokeo ya Medeama, na badala yake tunelekeze nguvu katika michezo ya ligi, tutakaoanza kucheza dhidi ya Mtibwa.

“Ninataka kuona tunaendelea na kasi ya ushindi mkubwa na soka safi la kuvutia, kama tulivyoanza katika michezo ya awali ya ligi ambayo tulipata ushindi na soka safi litakalowafuraisha mashabiki wetu,” alisema Gamondi.

STORI NA WILBERT MOLANDI

Leave a Comment