
Klabu ya Yanga imetangaza kuwa Mkurugenzi wa Matawi na Wananchi, Haji Mfikirwa amemaliza mkataba wake wa kuitumikia Klabu hiyo hivyo anaondoka huku ikimshukuru kwa utumishi wake klabuni hapo na kumtaka Kila la Kheri katika maisha yake nje ya klabu hiyo.
Taarifa ya Idara ya Habari na Mawasiliano Young Africans SC imebainisha kuwa Mfikirwa amehudumu klabuni hapo katika kipindi cha miaka mitatu akishika nafasi mbalimbali, ikiwemo Mkurugenzi wa Fedha na Kaimu Mtendaji Mkuu.
“Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa shukrani za dhati kwa Ndg. Haji Mfikirwa kwa utumishi wake na tunamtakia kila la heri na mafanikio katika maisha na kazi zake nje ya Klabu yetu.” imesema taarifa hiyo.
