×

Usiyoyajua Kuhusu Dk Emmanuel Nchimbi Katibu Mkuu Mpya CCM – Video

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Mstaafu Dkt. Emannuel Nchimbi.

Taarifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeeleza kuwa, Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekutana Januari 15, 2024 huko mjini Unguja visiwani Zanzibar na kumteua Dk Emmanue Nchimbi kwa Katibu Mkuu Mpya wa chama hicho.

Katibu Mkuu huyo mpya wa anachukua mikoba ya Daniel Chongolo aliyejiuzulu wadhifa huo Novemba, mwaka jana.

Chongolo aliachia wadhifa huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuchafuliwa kwenye mitandao ya kijamii kwa tuhuma mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara, Abdulrahman Kinana akipeana mikono na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi alipowasili Katika Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

Nchimbi anachukua nafasi hiyo baada ya kustaafu ubalozi wa Tanzania nchini Misri mwaka jana.
Mbali na kuhudumu nafasi ya ubalozi nchini Misri pia aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil.

Pia mbali na kuwa balozi katika nchini hizo, Nchimbi amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za Serikali na ndani ya CCM tangu akiwa kijana kama ifuatavyo;

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Kassim Majaliwa akimpa mkono wa Pongezi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Emmanuel Nchimbi, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Januari 15, 2024 Kisiwani Zanzibar.

Nchimbi aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini kupitia CCM kuanzia mwaka 2005 hadi 2015 sambamba na kuhudumu nafasi za uwazi katika wizara tofauti.

Kabla ya hapo aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara kuanzia mwaka 2003 hadi 2005.

Nchimbi alituliwa na Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk John Pombe Magufuli kuwa Balozi wa Brazil Desemba 3, 2016, kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan hajamhamishia kuhudumu Misri.

Kwa wasiomjua, Nchimbi amezaliwa Desemba 24, 1971 mkoani Mbeya.

Elimu yake ya msingi aliianizia jijini Dar es Salaam katika Shule ya Msingi Oysterbay kati ya mwaka 1980 hadi 1986.

Nchimbi alipelekwa katika sekondari ya Uru kati ya mwaka 1987 hadi 1989 (kidato cha kwanza hadi cha tatu kisha alihamishiwa Sekondari ya Sangu na kuhitimu kati ya mwaka 1989 hadi 1990.

Nchimbi alisoma Sekondari ya Forest Hill ya jijini Mbeya kwa masomo ya kidato cha tano na sita kati ya mwaka 1991 hadi 1993.

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro na kuhitimu stashahada ya juu ya utawala kati ya mwaka 1994 hadi 1997.

Wakati akihitimu masomo ya elimu ya juu, Nchimbi alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na mwaka 1998 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa.

Leave a Comment