×

Yanga Yathibitisha Kumsajili Mshambuliaji Joseph Guede

Joseph Guede

Klabu ya Yanga imethibitisha kumsajili mshambuliaji Joseph Guede ambaye amekuwa mchezaji huru tangu Septemba 2023 baada ya kuachana na klabu ya Tuzlaspor inayoshiriki Ligi daraja la pili Nchini Uturuki.

Guede (29) raia wa Ivory Coast amewahi kuchezea pia katika klabu ya FAR Rabat ya Morocco kabla ya kupelekwa kwa mkopo UAE kunako klabu ya Emirates Club ya Jumuiya ya falme za Kiarabu.

Leave a Comment