×

Watu 90 Wapoteza maisha Nchini Marekani kufuatia dhoruba kali ya msimu wa baridi

Takriban watu 90 wametipotiwa kupoteza maisha Nchini Marekani baada ya nchi hiyo kukumbwa na dhoruba kali ya msimu wa baridi kwa wiki moja iliyopita.

Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika ni pamoja na jimbo la Tennessee ambako takriban watu 25 wamefariki huku watu 16 wakipoteza maisha katika Jimbo la Oregon ambapo kuna hali ya hatari kufuatia dhoruba kali za barafu. Makumi ya maelfu ya watu pia wanasalia bila umeme katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

Hali ya barafu inatarajiwa kuendelea hadi katikati ya wiki. Jumla ya vifo 89 vinavyohusiana na hali ya hewa vimerekodiwa kote nchini katika wiki iliyopita, kulingana na hesabu iliyothibitishwa na CBS.

Wakati idadi ya vifo imekuwa kubwa zaidi katika majimbo ya Tennessee na Oregon, vifo pia vimeripotiwa katika majimbo ya Illinois, Pennsylvania, Mississippi, Washington, Kentucky, Wisconsin, New York, New Jersey na kwingineko.

Katika tukio moja huko Portland, Oregon Jumatano iliyopita, watu watatu walipigwa na radi hadi kufa wakati upepo mkali uliposababisha njia ya umeme kuanguka na kuligonga gari walimokuwa wakisafiria huku mtoto mchanga aliyekuwa kwenye gari akinusurika.

SAMATTA ANA BIFU na KOCHA? MBONA HAKUMPA MKONO ALIPOFANYIWA SABU – MWENYEWE AJIBU…

Leave a Comment