
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametoa siku 30 kwa Mkandarasi Halem Construction kukamilisha ujenzi wa Mradi wa Maji Navanga.
Waziri Aweso ameyasema hayo alipofika Jimbo la Mtama kutembelea na kukagua mradi wa Maji ukanda wa Navanga unaotekelezwa katika kata 5 zilizopo katika Wilaya ya Lindi ambao kwa sasa umefikia asilimia 90.

Mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 utahudumia vijiji hivi vyenye jumla ya watu wapatao 17,015 wenye wastani wa mahitaji ya Maji lita 425,375 kwa siku.
Akihitimisha hotuba yake Waziri Aweso amefikisha salamu za Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe Nape Moses Nnauye aliemuomba kwa dhati kufika Navanga na alieupigania mradi huo kwa dhati mpaka ulipofikia hatua hii ya kukamilika.