Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inatarajia kutangaza vitalu 24 vya Mafuta na Gas asilia baada ya kukamilika kwa Utafiti nchi kavu na baharini na kubainika maeneo hayo yana viashilia upatikaji wa nishati hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa PURA ,Mhandisi Charles Sangweni,alisema hayo katika uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi ulifanyika mjini Morogoro. Mhandisi Sangweni,
alisema kwa kuanzia wanategemea vitalu hivyo baharini vitakuwa 10 na nchi kavu vitakuwa 14 na kwa sasa wapo katika hatua ya kumpata mshauri elekezi kwaajili ya kwenda kuweka mipaka pamoja na alama katika maeneo hayo yatakayotangazwa.
” Tunategemea kazi hii tutaanza rasmi mwezi wa sita ,lakini kwanza lazima unaanza kuinadi kwenye mikutano na makungamano ya Kimataifa inayohusiana na masula ya Mafuta na Gas na matamanio yetu mwanzoni mwa mwaka 2025 tutajadiliana na wawekezaji ili kuingia mikataba” alisema Mhandisi Sangweni.
Mkurugenzi Mkuu wa PURA alisema miongoni mwa kazi yao ni kufanya utafiti na tafiti za awali zinaonyesha zaidi ya asilimia 50 la nchi limeonekana kuwa na viashiria vya mafuta.
Alisema PURA imeona ni wakati muafaka wa kuongeza kasi ya kufanya utafiti kutokana na dalili ya maeneo mengi yanafafan na dalili zilizoonekana nchini Uganda, Kenya eneo la Turkana ambapo yamegundulika mafuta na kuna dalili kama hizo katika bonde la Ufa. Mhandisi Sangweni, alisema Serikali kupitia
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Athuman Mbuttuka ameagiza PURA kusimamia zoezi la ugawaji wa vitalu vya Mafuta na Gas linasimamiwa na kukamilika kwa maslahi mapana ya Taifa ili kuhakikisha serikali inapata maslahi yake
. Amesema ugawaji huo uhakikishe unazingatia sheria pamoja na kuwapa mafunzo watumishi watakaofanya kazi hiyo ili waweze kujua wajibu wao na kutekeleza malengo waliokabidhiwa na serikali.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(TUCTA) Henry Mkunda amesema alipongeza PURA kwa kutekeleza takwa la kisheria la kufanya mikutano ya Baraza la wafanyakazi mara mbili kwa mwaka.
Amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, weledi na kujituma na kuepuka ubadhilifu ili kuhakikisha taasisi inapata maendeleo huku ikiweka mahusinao mazuri baina ya mwajili na wafanyakazi.