Msanii wa Bongo Muvi Steve Nyerere mara baada ya kufika msibani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, amefanya mahojiano na waandishi wa habari na kueleza kuwa Lowasa alikuwa mwanasiasa wa kuigwa hivyo basi anawaalika wasanii wote wajumuike kwenye safari yake hiyo ya mwisho.