
Kilimanjaro, 25 Februari 2024: Mbio za Tigo Kili International Marathon Km 21, leo imetimua vumbi kuanzia kwenye Uwanja wa Chuo Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro na viunga vyake ambapo kwa upande wa wanaume Mtanzania Faraja Damas Lazaro ndiye aliyeibuka mshindi na Wanawake Failuna Abdi Matanga ambaye naye Mtanzania.
Mbio hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo Dk. Damas Ndumbaro ambaye aliipongeza Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo kwa kuendelea kuisapoti mbio hiyo na kusema kitendo hicho ni kurudisha fadhila kwa jamii.
Pamoja na kuipongeza Tigo, Dk Ndumbaro aliwapongeza wakimbiaji wote waliokimbia mbio hiyo pamoja na wale waliokimbia Km 42 na mbizo ya kujifurahisha za Km 5.
Wengine walioingia tano bora kwenye mbio hiyo kwa upande wa wanaume ni Peter Mwangi kutoka Kenya aliyeshika nafasi ya pili, watatu ni Kenedy Abel wanne ni Boay Dawii na watano ni Aloyce Simbu washindi wote kutoka Tanzania kasoro mshindi wa pili.
Kwa upande wa wanawake waliomfuatia Failuna ni Neema Kisuda, Neema Festo, Neema Msuadi na Sara Ramadhani wote kutoka Tanzania.
Akizungumza kwenye kuhitimisha mbio hiyo, Afisa Mkuu wa Fedha Tigo, CPA Innecent Rwetabura alisema; Awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na kutuwezesha kuwepo hapa leo.
Pili, naomba nikushukuru mgeni rasmi kwa kutoa muda wako na kuwa nasi na kushuhudia mbio za Kilimanjaro International Marathon ambazo leo zimefikisha miaka 22 yenye mafanikio makubwa.
- Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza waandaji wa mbio hizi kwa kuendesha mbio hizi kwa weledi mkubwa na kuzifanya kuwa za viwango vya kimataifa.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
- Tangu mwaka 2015, Tigo tumekuwa wadhamini wa mbio za Kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili International Half Marathonili kukuza utalii wa michezo, kuibua na kukuza vipaji vya riadha na kuongeza chachu kwenye sekta ya utalii wa ukanda huu wa Kaskazini ikiwemo kuutangaza urithi wetu wa mlima Kilimanjaro.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
- Malengo yetu yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani tumekuwa na wanariadha wanaoshiriki na kushinda mbio za kimataifa ambao wamekuwa washindi wa Tigo Kili International Marathon. Sote ni mashahidi wa ongezeko la wanariadha na utalii wa michezo kwa ujumla na kupelekea mwaka huu wa 2024 kuongeza idadi ya washiriki wa Tigo Kili International Half Marathon kufikia zaidi ya watu
- Sambamba na hili, Tigo tumeongeza Zawadi za washindi kufikia shilingi milioni 19,420,000/- ili kuvutia wanariadha wengi zaidi kushiriki. Mbali na hapo tumetoa pia zawadi maalum kwa mshindi wa kwanza Mtanzania.
- Mafanikio haya pia yanaleta hamasa kwenye sekta ya uchumi kwa kuwa mji wa Moshi unahudumia watu wengi hivyo kunufaisha wafanyabiashara na watoa huduma mbali mbali. Mtakubaliana na mimi kuwa, mbio hizi zimekuwa ni chachu ya kuanzishwa kwa mbio nyingine nyingi nchini Tanzania.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi:
- Ninapenda kukuhakikishia mheshimiwa Waziri na kila mmoja aliyepo hapa kuwa, Tigo tumejipanga kuendelea kutoa huduma bora kwa watanzania na wateja wetu nchi nzima.Pia, mbali na mikakati yakibiashara, tunaendeleza ubunifu na mipango yenye tija kwa Taifa ili kushiriki kimalifu katika ustawi wa jamii na uchumi kwa ujumla.
- Mwaka 2022, Tigo tulianza mradi wa kuboresha miundombinu yetu ya mawasiliano nchi nzima ambapo kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2024, tutakuwa na teknolojia ya 4G nchi nzima na 5G katika miji mikubwa ikiwemo Moshi. Mradi huu utatugharimu zaidi ya TZS trilioni moja (1 trillion) kwa kipindi cha miaka mitano.
- Ninapenda kuwafahamisha kuwa kwa hapa mjini Moshi hadi sasa tunajivunia minara mitatu(3) ya 5G ambayo ipo KCMC, Shanty townnaMbuyuni/Korongoni). Uwekezaji huu ambao unafanyika nchi nzima, umetupatia tuzo ya kimataifa ambapo Tigo tumedhibitishwa na Ookla, kama Mtandao wenye kasi zaidi Tanzania kwa mwaka 2023.
- Hata hivyo kupitia ripoti ya robo ya mwisho ya mwaka jana (Q4 -2023), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imethibitisha kuwa Tigo ni mtandao wenye huduma bora zaidi Tanzania (Quality of Service).
Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
- Tigo mwaka huu tumeweka Wi-Fi spots BURE, katika maeneo mabalimabili hapa mjini Moshi kama vile; Amuz Bar, Redstone Night Club, Moshi Pazuri, Kili Home pamoja na Moshi Clubili kuwafanya washiriki wa Tigo Kili International Half Marathon waweze kuendelea kuwasiliana familia zao huku wakishuhudia maboresho tuliyoyafanya. Tunaamini wote walioweza kufurahia intaneti yetu yenye kasi zaidi Tanzania watawaambia wanafamilia na marafiki zao wajipatie laini za Tigo.
- Napenda kutoa shukrani za dhati kwa mara nyingine tena kwa waandaji wa mbio hizi, wafanyakazi wa Tigo, wadhamini wenzetu kwa kuandika historia nyingine tena mwaka huu kwa kufanikisha Tigo Kili International HalfMarathon 2024.
- Tunathamini kujitoa kwenu kwa hali na mali, kuhakikisha kila mshiriki ameweza kutimiza lengo lake huku akifurahia ukarimu wa watu wa Kilimanjaro.
- Kipekee nnapenda kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na uongozi mzima wa Mkoa huu kwa mapokezi mazuri kila mwaka. Mmetuonyesha ukarimu wa hali ya juu sana, Asanteni sana!
- Mwisho ningependakuwashukuru washiriki wote wa Tigo Kili International HalfMarathon 2024 kwa kushiriki kikamilifu kutangaza utalii wa nchi yatu, kuimarisha afyana kuchangia uchumi wa mkoa wa Kilimanjaro. Kwa pamoja tumeweza kutengeneza kumbukumbu zisizofutika katika kila hatua tuliyopitia na kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa za kipekee, tukutane tena TigoZantel Zanzibar International Marathon, mwezi Octoba, 2024.