Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya, Mjini na Mwanahip hop, Joseph Mbilinyi na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Muliro Jumanne leo walibambana ‘laivu’ Uwanja wa Uhuru jijini Dar ambapo mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu Ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ulikuwa ukiagwa.
Sugu alifika uwanjani hapo kama waombolezaji wengine ambapo baada ya kutoka heshima za mwisho ndipo akakutana na afande Muliro ambaye walianza kupiga stori huku wakikumbushiana jinsi wanavyopelekeshana puta kwenye visanga mbalimbali kama vile maandamano na mengineyo.

Tukio la wawili hawa kupiga stori ‘kishkaji’ liliwavutia ambapo wengine waliionekana kuwazunguuka wakati wakipiga stori zao ndipo paparazi wetu naye akaona asiliache tukio hilo. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL