
Katibu mkuu chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu leo Machi 22, 2024 amefanya mahojiano na @255globalradio na @globaltvonline na kudai kuwa wao kama chama watajiondoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar endapo mambo yaliyoandikwa na Maalim Seif hayatafanyiwa kazi kwani wamevumilia kwa muda wa miaka minne sasa.
Ado ameendelea kuiambia Globa Tv kuwa wao kama chama wataonana na viongozi wa juu kuwasilisha suala lao.