×

Thea – Sitaki Kupostiwa Nikifa, Nimekaa Miaka 20 Bila Kupata Mtoto

Msanii mkongwe kwenye tasnia ya uigizaji, Salome Ndumbagwe @thea ametoa tahadhari kuwa ikitokea amefariki, hataki kupostiwa na mtu yeyote ambaye hakuwahi kumposti kupitia kazi yake wala anachofanya.

Amesema mtu ambaye hajawahi kumpost kupitia kazi zake akampost akifikwa na umauti, atafufuka kwenye jeneza na itakuwa ni maajabu ya kwanza kutokea.

“Mimi sitaki kabisa uniposti nikiwa nimekufa kama unapenda kazi zangu niposti nione wakati niko hai, sasa ukiposti nimekufa naonaje yaani naomba kabisa kutachimbika na tena kama Johari asiniposti kabisa nikifa,” alisema Thea.

Leave a Comment