PM Majaliwa Ajionea Kifaa cha Mawasiliano ya Intaneti (router) Cha Airtel Chenye Uwezo wa Kasi ya 5G
Global Publishers May 14, 2024 0 Comments
SHARE THIS:
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akiangalia kifaa cha mawasiliano ya Intaneti (router) chenye uwezo wa kasi ya 5G, huku Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano (katikati), akitoa maelezo kuhusu kifaa hicho, shughuli za Airtel na maendeleo ya Kampuni hiyo hususani mradi wa ujenzi wa minara 758, ambayo Airtel imefikisha zaidi ya asilimia 70 ya minara 187 iliyopewa kujenga. Ilikuwa ni katika maonyesho ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Habari, Taasisi zake na wadau wa Mawasiliano, katika Viwanja vya Bunge, Dodoma. Hii imeenda sambamba na uwasilishwaji wa bajeti ya Wizaya ya Habari. Katikati ni Waziri wa Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia). Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Airtel, Serikalini, Bi. Jennifer Mbuya.Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano (katikati), kuhusu shughuli na maendeleo ya Kampuni hiyo hususani mradi wa ujenzi wa minara 758 ambayo Airtel imefikisha zaidi ya asilimia 70 ya minara 187 iliyopewa kujenga. Ilikuwa ni katika maonyesho ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia na Habari, Taasisi zake na wadau wa Mawasiliano, katika Viwanja vya Bunge, Dodoma, jana. Hii imeenda sambamba na uwasilishwaji wa bajeti ya Wizaya ya Habari. Katikati ni Waziri wa Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kulia). Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Airtel, Serikalini, Bi. Jennifer Mbuya.