
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema serikali imedhamiria kuleta mapinduzi ya Kidigitali kupitia Mpango wa Miaka 10 ya Uchumi wa Kidigitali ulioanza kutekelezwa mwaka 2023 mpaka mwaka 2033.
Waziri Nape ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma na kueleza hatua ambazo wizara yake imeanza kuzitekeleza katika mpango huo.