×

Amazing Tanzania Yazinduliwa Kwa Kujaza Mastaa Beijing Opera House

Nyota wa filamu nchini China Jin Si Sui, akijulikana zaidi kwa jina la Jin Dong, ambaye ndiye mgeni mashuhuri katika filamu ya Amazing Tanzania anayeonekana kuoneshwa uzuri wa Tanzania katika filamu hiyo, ni miongoni mwa mastaa wa hapa waliohudhuria uzinduzi uliowavuta viongozi, wasanii na wadau mbalimbali wa utalii.

Huku wakipiga makofi na mara nyingine kushangazwa na uzuri wa Tanzania katika sehemu mbalimbali za filamu hiyo, Wachina wengi waliohudhuria uzinduzi huo kwenye ukumbi wa National Opera House jijini Beijing, wameonekana kufurahia vitu kama wanyama wengi waliooneshwa kwenye filamu, mbizi za vijana wa makachu Zanzibar, “Selfi” aliyopiga Rais Samia na zaidi kushangazwa na uwepo wa makundi ya ndege aina ya herode (flamingo) ambao ni ndege adimu na alama ya upendo katika utamaduni wa Wachina.

Pamoja na Jin Dong anayejulikana kwa filamu zake kali kama “Legend of Entrepreneurship”(2012), “The Disguiser” (2015), “Candle in the Tomb” (2016), “Surgeons” (2017) and “The First Half of My Life” (2017), watu wengine mashuhuri waliohudhuria ni: mwanasiasa mashuhuri na Waziri wa Utalii na Utamaduni wa China Bw. Sun Yeli, Mi Qianming mchoraji mashuhuri China na Wan Linmei, mwanamuziki. Mawaziri wa Utalii, Utamaduni kutoka Tanzania Bara pia wamehudhuria uzinduzi huo na Waziri wa Michezo kutoka Zanzibar.

Ni dhahiri “Mailii Tansaniya” (Jina la Kichina la Amazing Tanzania), ni lango jingine la kuifungua Tanzania duniani na Uchina.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameungana na Viongozi pamoja na Waumini wa Kanisa Katoliki katika Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Dar es salaam Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap inayofanyika Msimbazi Centre Jijini Dar es salaam tarehe 16 Mei 2024.

Leave a Comment