×

Nesi Aliyempokea Tundu Lissu Akiwa Mahututi Afunguka Mazito – Video

Tangu kutokea kwa tukio la Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kupigwa risasi jijini Dodoma, hatimaye leo amekutana na muuguzi Veronica Alexander ambaye ameeleza kwamba ndiye aliyekuwa wa kwanza kumpokea alipofikishwa katika Hospitali ya General, Dodoma baada ya tukio hilo.

Mwanamama huyo amesimulia kila kitu kilichotokea mpaka kauli ya mwisho ya Lissu aliyoitoa kabla hajapoteza fahamu.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Kijiji cha Ihumwa, Dodoma kwenye msiba wa mchungaji anayedaiwa kujinyonga kisa kikitajwa kuwa ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni.

Leave a Comment