
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa na viongozi mbalimbali aliyowateua hivi karibuni, katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumatano, Juni 2, 2021.
Miongoni mwa walioapa ni Mbunge wa Newala Mjini, Kapteni George Mkuchika ambaye ameapishwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu – Kazi Maalum.
Ngusa Samike aliyekuwa Katibu wa Hayati Rais Dkt. John Magufuli ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza na wengine.