
Klabu ya Azam FC imemtambulisha, kiungo Ever Meza kama mchezaji mpya klabuni hapo aliyesajiliwa kutoka klabu ya Leonnes ya Colombia. Meza alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Alianza FC ya huko huko Colombia.
Ever William Meza Mercado raia wa Colombia aliyezaliwa Julai 21, 2000 amesaini mkataba wa miaka minne utakaomuweka Azam Complex hadi mwaka 2028.
