
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mataves, katika eneo la Kitongoji cha Kisongo, Kijiji cha Ngorbob, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, na kusikiliza kero zao na kuzitafutia majawabu, ambapo pia alizindua Shina la Wakereketwa wa CCM Akinamama Wajasiriamali wa Soko la Kisongo, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, leo Jumapili Juni 2, 2024.
Akizungumza na wananchi amesema Watanzania wote wana sifa sawa, tuendelee kusimamia umoja wa nchi yetu, tuendelee kusimamia mshikamano na hivyo Watanzania ni kitu kimoja. Watanzania wote ni ndugu wakatae kugawanywa kikabila, mkatae kugawanywa kidini, mkatae kugawanywa kwa maeneo ya nchi yetu,” Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Kisongo, Kijiji cha Ngorbob, Kata ya Mataves, Wilaya ya Arumeru.