×

Yanga yatwaa ubingwa wa Shirikisho Tanzania ikiandikisha rekodi – Video


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga wamefanikiwa kuchukua taji lao la pili kwa msimu wa 2023/24 baada ya kuwalaza Azam FC kwenye fainali ya kombe la shirikisho usiku wa kuamkia leo huko visiwani Zanzibar.

Yanga ambao wamechukua taji lao la nane la shirikisho tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo iliwalazimu kupata ushindi huo kwa chagamoto ya mikwaju ya penati 5-6 baada ya dakika 120 kuisha 0-0

Licha ya kukosa penati mbili za kwanza Yanga walifanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya winga wa Azam, Iddy Suleiman kupaisha juu ya lango penati yake.

Ikiwa hii ni mara ya nane kuchukua taji hilo lakini Yanga imejiandikia historia yake baada ya kuchukua kombe hilo mara tatu mfululizo mwaka 2022, 2023 na 2024.

MWAMNYETO ASHINDWA KUJIBU HAYA – “SINA UHAKIKA na MSIMU UJAO – MUDA HAUJAFIKA BADO”……

Leave a Comment