
Huduma zote za Kivuko cha MV. Kigamboni kinachovusha Abiria kati ya Magogoni Kivukoni na Kigamboni zimesitishwa kuanzia Juni 7, 2024, tangazo hilo limetolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA)
Taarifa ya TEMESA imeeleza Kivuko hicho kinasimama kutoa Huduma kwaajili ya kwenda kufanyiwa Ukarabati mkubwa kwa lengo la kukiwezesha kutoa huduma Bora kikiwa katika hali ya Usalama
TEMESA imeeleza Abiria wenye Magari wanashauriwa kuanza kutumia njia ya Daraja la Mwalimu Nyerere ili kuepuka Msongamano wakati ambapo huduma za Kivuko zitaendelea kutolewa na MV. Kazi na Sea Taxi