
BEKI wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari bado hajafanikiwa kuongezewa mkataba mpya na timu yake.
Kibwana mkataba wake na Yanga umetamatika rasmi Juni na kwa sasa ni mchezaji huru.
Kibwana ndani ya Yanga ameshindwa kupenya katika kikosi cha Kwanza mbele ya Yao Kwasi ambaye amekuwa akianza mara kwa mara.
Akizungumza juu ya Mkataba wake Kibwana amesema kuwa “Mkataba wangu umetamatika tayari ndani ya Yanga na kinachoendelea kwa sasa ni mazungumzo na uongozi wangu.
“Kipaumbele kikubwa kwa sasa ni Yanga kwa kuwa ndio nipo lakini kama itapatikana ofa nzuri kutoka kwa timu nyingine basi naweza kuondoka,” Kibwana