
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka DART umewaarifu watumiaji wa mabasi ya – Mfumo wa DART kuwa leo, Juni 19, 2024, Barabara ya Jangwani imefungwa kutokana na mafuriko.
Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma cha DART ya leo Juni 19, 2024 imebainisha kuwa Mabasi kwa njia za Kimara hadi Kivukoni na Gerezani yanaishia Magomeni Mapipa huku huduma ya usafiri wa Mabasi ya DART ikiendelea kutolewa kwa njia ya Morocco kwenda Kimara; na eneo la katikati ya jiji kwa njia ya Muhimbili na Gerezani.
Aidha, huduma za Mabasi katika mfumo wa DART zinaendelea kama kawaida katika Njia Mlishi ya Kimara hadi Mbezi, Kimara hadi Kibaha, na Kimara hadi Mloganzila.