×

Bilionea Atoa Mchango wa Bilioni 131 kwa kampeni ya Trump

Bilionea Timothy Mellon.

TIMU ya kampeni za urais za Donald Trump imepokea jeki ya $50m (Tsh 131,250,000,000.00 ) kutoka kwa bilionea Timothy Mellon.

Hazina ya Super-Pac inayoitwa “MAGA Inc” ilifichua kwa Tume ya Shirikisho ya Uchaguzi kwamba ilichukua zaidi ya $68m kutoka kwa wafadhili mwezi uliopita.

Reuters iliripoti kuwa Mellon, mrithi wa familia ya benki ya Mellon iliyoko Pittsburgh, alitoa $50m. $10m nyingine zilitoka kwa mabilionea Liz na Dick Uihlein.

Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba  Mellon alituma mchango huo siku moja baada ya Trump kuhukumiwa kwa mashtaka 34 ya kughushi rekodi za kibiashara katika kesi yake ya uhujumu uchumi ya New York.

Bw Mellon pia amekuwa mfadhili mkubwa zaidi wa mgombeaji huru wa urais Robert F Kennedy Jr, akitoakwaKennedy Super-Pactakriban$20m.

Donald Trump

Super-Pacs ni “kamati za hatua za kisiasa” huru ambazo zinaweza kukusanya kiasi kisicho na kikomo cha pesa kusaidia mgombeaji wa uchaguzi.

Mchango wa Mellon umesaidia washirika wanaomuunga mkono Trump kuwashinda washirika wa Rais wa MarekaniJoe Biden kwenye kampeni katika wiki za hivi karibuni.

Wakati huo huo, Reuters iliripoti kwamba bilionea Mike Bloomberg ametoa karibu $ 20m kwa Super-Pac inayounga mkono Biden.

Mchango wa Bw Bloomberg ulijumuisha $19m kwa kikundi huru cha wafuasi wa Biden kinachojulikana kama Future Forward au FF PAC.

$900,000 zaidi zilitolewa kwa Mfuko wa Ushindi wa Biden, ambao ni muungano wa kampeni ya Biden na kamati za Chama cha Democratic.

Kampeni ya Biden haikujibu mara moja ombi lakutoa maoni.

Siku ya Alhamisi, kampuni inayomuunga mkono Kennedy Super-Pac iliripoti kwamba ilichukua karibu dola 280,000 pekee mwezi uliopita, na hakuna hata moja iliyotoka kwa Bw Mellon.

MSIBA wa MAMA wa MISS TANZANIA AMISUU MALICK – MWANAYE AELEZA – “PESA MLIZOCHANGA TATOA SADAKA”…

Leave a Comment