×

Yanga: Tutafanya usajili wa kishindo Ali Kamwe Afunguka

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa utafanya usajili wa kishindo katika dirisha kubwa la usajili ambalo limefunguliwa Juni 15 2024.

Ikumbukwe kwamba Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24 wataipeperusha bendera ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua kazi kubwa inapaswa kufanyika ili kupata kikosi bora zaidi jambo ambalo linafanyiwa kazi.

“Tutafanya usajili wa kishindo tunatambua kwamba ili kuwa bora ni muhimu kuwa na kikosi imara jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa umakini mkubwa.”

MWENYEKITI na DIWANI wa MTAA ALIPOUAWA MTOTO wa FORM 3 WAFUNGUKA – ”VIJANA WANATUSUMBUA”…

Leave a Comment