
Wamiliki wa magari wanaodaiwa ushuru wa maegesho ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kulipa ushuru wa maegesho (Parking) haraka kabla ya Juni 30, 2024 vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Tamko hili limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, Juni 20 2024 alipokuwa katika Kikao na Viongozi wa Madereva na Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri na Daladala. Alisema, “Natoa wito kwa wale wote wanaodaiwa kodi za maegesho ya magari, watumie kipindi hichi cha wiki moja kulipa madeni yote ya kodi wanazodaiwa kwa wakati.”