×

Rais wa Malawi Amteua Waziri wa Maliasili kuwa Makamu wa Rais

Michael Bizwick Usi

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amemteua Waziri wa Maliasili Michael Bizwick Usi kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo.

Rais Chakwera amefanya uteuzi huo baada ya aliyekuwa Makamu wake Saulos Chilima kufariki katika ajali ya Ndege.

Ni mtunzi mashuhuri wa tamthilia, mwigizaji, mchambuzi wa masuala ya kijamii na mwanaharakati wa haki za kiraia.

Usi amehudumu kama Makamu wa Rais wa vuguvugu la mabadiliko la Chilima (UTM) tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2018.

Alijiunga na Baraza la Mawaziri la Rais Chakwera mnamo 2020 wakati UTM ilipoingia katika Muungano wa uchaguzi na Chakwera’s Malawi Congress Party (MCPP) katika uchaguzi wa 2020.

NEEMA kwa WALIKOSA NAFASI ya KUJIUNGA JKT kwa MUJIBU wa SHERIA – BRIGEDIA MABENA AELEZA HAYA…

Leave a Comment