×

Tanzania na Guinea-Bissau Wasaini Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embaló leo tarehe 22 Juni, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Embaló yuko nchini kwa ziara ya kikazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Samia Suluhu Hassan Akimpokea Rais wa Jamhuri ya Guniea-Bissau  Umaro Sissoco Embaló leo tarehe Juni 22, 2024 Ikulu Dar es Salaam .

Rais Samia na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, wameshuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya Nchi mbili, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ameweka saini kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa na Jamii wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Carlos Pinto Pereira akitia saini kwa upande wa nchi yake.

Umaro Sissoco Embaló aliyewasili kwa ziara ya kikazi kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rais Umaro Sissoco Embaló akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Rais Samia akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake.
Rais Samia akimkabidhi mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embaló zawadi ya vitabu vya Lugha ya Kiswahili.
Rais Samia akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embaló.
Rais Umaro Sissoco Embaló akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Rais Samia Ikulu Jijini Dar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló, wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya Nchi mbili, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akitia saini kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa na Jamii wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Carlos Pinto Pereira akitia saini kwa upande wa nchi yake.

Leave a Comment