Sakata la mikopo inayotolewa mitandaoni na baadaye waliokopeshwa wakishindwa kulipa kudhalilishwa kwa watu wao wa karibu kutumiwa meseji au kupigiwa simu, limetua bungeni jijini Dodoma ambapo Spika Tulia Ackson ametaka kusikia kauli ya serikali.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akatoa msimamo wa serikali na kueleza kuwa jambo hilo ni kinyume cha sheria na serikali inalifuatilia kwa karibu.