
RAIS John Magufuli amepokelewa kwa shangwe na vifijo wakati akiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika kusherehekea mwaka wa 58 tangu Tanganyika (Tanzania Bara) ipate uhuru ambapo kitaifa sherehe hizo zinafanyika jijini humo.

Aliingia uwanjani hapo saa 3:14 asubuhi leo Jumatatu, Desemba 9, 2019, akiwa kwenye gari la wazi akiongozwa na pikipiki nane gari moja mbele na nyingine nyuma.
Aliingia kupitia upande wa kushoto wa uwanja na kuuzunguka akiwapungia mikono wananchi waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.