Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini kupitia Chadema, Mchungaji Peter Msigwa ameeleza sababu mbalimbali zilizomfanya akachukua uamuzi wa kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), kubwa ni utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuwaunganisha Watanzania.
Mchungaji Msigwa amesema hayo leo Jumapili, Juni 30, 2024, saa chache baada ya kujiunga na CCM mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyikia Ofisi Ndogo za CCM, Lumumba akiwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, Mchungaji Msigwa Amesema ameridhishwa na utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuwaunganisha Watanzania.