
Benki ya Equity inayojihusisha na utoaji wa huduma mkbalimbali za kifedha jana imezindua banda lake la kutolea huduma kwenye Viwanja wa Maonesha ya Kibiashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba.
Akizungumza baada ya kukata utepe kwenye uzinduzi huo Meneja Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki hiyo Leah Ayub amesema wanawakaribisha wateja wote kupata huduma zao za kisasa kwenye banda lao hilo.

Pamoja na mambo mengine kwenye banda hilo meneja huyo amesema wanatoa huduma zote za kibenki ikiwemo kuweka na kutoa pesa, huduma za mikopo na kuwataka wananchi kufika kwenye banda kujionea huduma hizo.
Meneja huyo alisema kuwa pia wana akaunti hiitwayo Hapo hapo Akaunti ambayo wameizindua wiki moja iliyopita.
Amesema; Akaunti hiyo ya Hapo hapo inatumiwa na wateja wetu kufungua akaunti kwenye simu zao za mkononi ambapo ni rahisi kabisa unachotakuwa ni kubonyeza *150*07# na utaipata huduma hiyo ya kidigitali zaidi.