
Dar es Salaam 2 Julai 2024: Kampuni ya Mtandao wa simu ya Tigo imewekeza huduma zake kwenye Viwanja vya Maonesho ya 48 Kimataifa ya Biashara hapa nchini maarufu kama Sabasaba ambapo wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali kwenye banda lao lililopo kwenye viwanja hivyo.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kwenye banda lao lililopo kwenye viwanja hivyo Mkurugenzi Tigo Kanda ya Dar es Salaam Kusini, Robert Kusirwa amesema katika maonesho hayo Tigo imekuja na huduma kedekede iliyowaletea wateja wake.

Pamoja na huduma hizo pia wanaendelea na Kampeni yao ya Sako kwa Bako na kuwaambia wateja wao kuwa wapo nao Sako kwa Bako.
Ameendelea kusema kuwa ukiingia katika banda lao la Tigo kuna huduma zote ambazo ungeweza kuzipata katika maduka yao mbalimbali yaliyopo nchi nzima kama vile kurejeshewa laini iliyopotea au kuharibika na nyinginezo.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa katika banda lao hilo zipo simu janja za bei nafuu kabisa kwa gharama ya kuanzia shilingi 180,000/ ukinunua kwa pesa taslimu na simu aina ya Enegizer kwa shilingi 189,000/ pamoja na hizo kuna simu zingine za aina mbalimbali kama vile Sumsung pamoja na ZTE.
Amesema simu hizo pia zinapatikana kwa mkopo na kuwataka wateja wasio na pesa taslimu kuondoa shaka na kusema kubwa zaidi katika banda lao hilo la Sabasaba.
Pia amesema ukiingia kwenye banda lao huachwi tupu kwani ukiwa na shilingi elfu moja itakuwezesha kutoka na zawadi mbalimbali zinazopatokana katika banda hilo kwa mchezo wa kubahatisha.
“Kuna mchezo wa kujaribu bahati ambao ukiweka shilingi elfu moja unaweza kupata sehemu ya zawadi kedekede tulizonazo zinazopatikana kwenye maduka yetu.
Pia karibuni mjionee maendeleo makubwa ya mtandao kwa ajili ya nyumba yako (home internet) ambayo ina kasi ya 5G.
“pamoja na hayo katika maeneo ya Mbweni na Bunju tuna teknolojia ya Fiber ambapo sisi ni mtandao wa kwanza kwa Tanzania kuweka huduma ya Fiber karibuni sana kwenye banda letu ujipatia huduma mbalimbali.” Alimaliza kusema Mkurugenzi huyo.