×

Waziri Jerry Silaa Aingilia kati mgogoro kati ya wakulima na wafugaji Chalinze – Video


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa ameingilia kati mgogoro kati ya wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Chamakweza wilayani Chalinze Mkoa wa Pwani ambapo wakulima wamemlalamikia waziri kuwa wafugaji baada ya kuvamia eneo hilo walianza kuwapiga na kuwafukuza ndani ya eneo lao.

Aidha Waziri Silaa baada ya kusikiliza pande zote mbili amesema ataagiza timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi kufika katika eneo hilo kujua ukweli wote ili maamuzi sahihi yaweze kutolewa.

Leave a Comment