×

Katibu Mkuu wa Utalii Atembelea Nyumba ya Kwanza ya Mwalimu Nyerere – Picha

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Julai 5, 2024 amefika Magomeni ilipo nyumba ya kwanza ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoijenga baada ya kuwa ameacha kazi Pugu Sekondari, akakaa chumba cha kupanga kujitafuta kama vijana wengine kwa miaka kadhaa kuanzia Machi 1955, hatimaye mwaka 1957 akaanza kujenga hapa na kuhamia mahali mwishoni mwa 1958.

Ni mahali hapa Magomeni ikiwa moja ya mitaa ya “kishua” wakati huo, Mwalimu alipofanya harakati zake za mwisho kuelekea uhuru na ni nyumba hii alipotokea asubuhi ya siku anakwenda kuapishwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika.

Pamesheheni historia adhimu ikiwemo vitu halisi alivyotumia Mwalimu kama samani, pasi, vyombo vya kupikia nk.
Kwa sasa hii ni Makumbusho rasmi na ipo wazi kutembelewa ikiwa chini ya @wizarayamaliasilinautalii Karibuni Magomeni Mtaa wa Makumbusho nyuma ya majengo ya Watumishi Housing.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi.

KIMENUKA SAKATA la SUKARI – SERIKALI YATOA TAMKO JIPYA – YAJIBU KILA KITU -MPINA ALIPULIWA

Leave a Comment