×

Azam Yathibitisha Kumsajili Mshambuliaji Adam Adam kwa mkataba wa mwaka mmoja

Klabu ya Azam fc imethibitisha kumsajili mshambuliaji Adam Adam kwa mkataba wa mwaka mmoja kutoka Mashujaa Fc.

Adam ambaye anarejea kwa Wanalambalamba hao baada ya kuwa nje kwa miaka 10 msimu liopita alifunga jumla ya mabao saba kwenye ligi alipokuwa na kikosi cha Mashujaa.

Adam ni zao la Akademi ya Azam FC, aliyojiunga nayo mwaka 2011-2014, ikiwa chini ya kocha Mhindi, Vivek Nagul na kubeba baadhi ya mataji kama vile U-20 Uhai Cup na Rollingstone.

Leave a Comment