×

Yanga Kumenyana na Vital’O ya Burundi, Azam dhidi ya APR Ligi ya Mabingwa

DROO ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekamilika ambapo Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo ya CAFCL wamebaini wapinzani wao.

Yanga itaanzia ugenini dhidi ya Vilal’O ya Burundi huku Wanalambalamba, Azam wakianzia nyumbani dhidi ya APR Fc ya Rwanda.

Mshindi wa matokeo ya jumla kati ya Yanga dhidi ya Vilal’O  atachuana na mshindi wa matokeo ya jumla kati ya SC Villa ya Uganda dhidi ya Commercial Bank ya Ethiopia kwenye raundi ya kwanza.

Aidha mshindi wa matokeo ya jumla kati ya Azam fc dhidi ya APR  ya Rwanda atakabiliana na mshindi kati ya JKU Fc ya Zanzibar dhidi ya Pyramids ya Misri.

HATUA YA AWALI

Vital’O 🇧🇮 vs 🇹🇿 Young Africans SC

Azam FC 🇹🇿 vs 🇷🇼 APR Fc

JKU FC 🇹🇿 vs 🇪🇬 Pyramids FC

Sc Villa 🇺🇬 vs 🇪🇹 Commercial Bank

Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zitapigwa kati ya Agosti 16 – 18 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Agosti 22 – 25, 2024.

Mechi mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Septemba 13-15, 2024 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Septemba 20-22, 2024.

MAUAJI MUDA HUU ARUSHA -WEZI WENGINE WANAPATA HUKUMU ya WANANCHI WENYE HASIRA KALI KATIKATI ya MJI..

Leave a Comment