×

Msigwa Awalipua Chadema, Akiri Upinzani Kupoteza Dira – Video

Ndani ya Miaka 20 nimejitahidi kuzungumza haki,demokrasia na Uhuru ndani ya Chama cha Chadema lakini sijaviona kwani mambo hayo imekuwa ni propaganda tu hakuna ukweli nami napenda ukweli.
Baada ya Dkt Samia Suluhu Hassan Kuingia madarakani alikuja na 4R  ambazo zilikuja kuibadilisha Nchi kabisa nasi Chadema tukabaki watu wakudandia hoja lakini tulipoona maridhiano tukamfuata Dkt Samia Suluhu Hassan lakini Mbowe baada ya kushughulika na Chama akawa unashughulika na Mboga zake na Maisha yake.
“Mimi nimejiunga na CCM baada ya kuona mambo tuliyopigania Kwa mda mrefu yanayafanywa kwa uweledi ndani ya CCM Mfano Mikutano ya hadhara, Uhuru wa Mawazo ,Uhuru wa Vyombo habari Katiba yenye kufuata Sheria lakini Chadema vyote hivyo havifuatwi nami roho yangu imenisuta kuikemea Serikali ya CCM wakati Sisi CHADEMA hatutendi haki”. Msigwa
Hivyo niwasisitize Ndugu zangu hasa Vijana tusome ramani Chadema imepoteza dira haieleweki inataka nini tuchague CCM ndo Chama kinachojidhughulisha na shida za watu Mie nimeona mfano hata kule Iringa mambo Makubwa yamefanyika ,Mchungaji Peter Msigwa amesema hayo akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Kawe Viwanja vya Panga Kinondoni.m

Leave a Comment