×

Rais Samia Aiagiza NFRA Ianze Kununua Mahindi kilo moja kwa shilingi 700 – (Video +Picha)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga tarehe 17 Julai, 2024.

Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) kuanzia kesho Julai 18, 2024 ianze kununua mahindi kilo moja kwa shilingi 700/- kutoka bei aliyoitangaza akiwa mkoani Katavi ya shilingi 600/-.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Mkoani Rukwa wakiwa katika uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani humo kwa ajili ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihitimisha ziara yake Mkoani humo tarehe 17 Julai, 2024.

Rais Samia amesema ametangaza bei hiyo mpya kutokana na maombi ya wakulima akisema huo ndio usikivu wa serikali.

“Kuna maombi yametoka hapa, nimepokea malalamiko nikiwa Katavi nikiwa kule nikapandisha bei (mia sita), nimekuja Rukwa malalamiko bado ni bei, nakuagiza waziri nendeni na bei ya mia saba. NFRA kuanzia kesho nunueni mahindi kwa mia saba… Ndugu zangu na huo ndio usikivu wa serikali,” amesema Rais Samia.

Rais Samia  akiwapungia mkono Wananchi wa Sumbawanga mara baada ya kuhutubia na kuhitimisha Ziara yake ya Kikazi katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa tarehe 17 Julai, 2024.

Leave a Comment