
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeundwa kwa mujibu wa Ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
Aidha, Ibara ya 88 ya Katiba inaunda Sekretarieti ya Bunge yenye jukumu la kuliwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake. Kwa msingi huo, Sekretarieti ya Bunge, inatangaza nafasi za kazi za Kada mbalimbali ili kuimarisha utendaji wake. Watanzania wote wenye sifa na uwezo wanaalikwa kutuma maombi yao ili kujaza nafasi za kazi kama zilivyoainishwa hapa chini:-
