
Kanisa la Mchungaji mmoja mwenye utata nchini Afrika Kusini limechomwa moto baada ya Mchungaji huyo kudaiwa kuvamia Shule moja ya msingi kwa mapanga na kuwaondoa wajukuu zake kwa nguvu.
Ripoti zinaeleza kuwa Kanisa la Mchungaji Paseka Motsoeneng lilichomwa moto na watoto wa shule wenye hasira siku ya Jumanne.

Mchungaji huyo ni maarufu kama nabii, anayejieleza kuwa na uwezo wa kufanya miujiza mingi ikiwemo kuponya magonjwa.
Siku moja kabla ya tukio hilo, video moja ilisambaa ikimuonyesha Mchungaji huyo akipunga mapanga juu wakati wa mabishano kati yake na Walimu yaliyotokea huko Katlehong, mji uliopo nje kidogo ya jiji la Johannesburg.
Mchungaji Motsoeneng na watu wengine watano wamekamatwa.