
Rais wa GSM Group, Ghalib Said Mohamed, amehudhuria hafla ya Yanga Day inayofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Ghalib aliwasili uwanjani na kupokelewa kwa hamasa na viongozi pamoja na mashabiki wa Yanga waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.
Mahudhurio yake yanaongeza uzito katika hafla hiyo ambayo imewakutanisha viongozi, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wa Yanga SC kwa ajili ya kuutambulisha msimu mpya wa 2026/27.
Yanga Day imekuwa pia sehemu ya mashabiki kupata fursa ya kuiona timu yao kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC, huku klabu ikitumia hafla hiyo kutambulisha mipango na matarajio yake kwa msimu ujao.
Uwanja wa Uhuru umeendelea kushuhudia shamrashamra za mashabiki waliovalia rangi za kijani na njano, huku wakisubiri matukio mbalimbali yaliyoandaliwa na klabu kwa ajili ya siku hiyo.

