×

Ofisi za TRA nchi Nzima Kuwa wazi Kuwahudumia Walipakodi siku ya Kesho

 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawataarifu Walipakodi na wananchi kwa jumla kuwa, Ofisi za TRA nchi nzima zitakuwa wazi kuwahudumia walipakodi siku ya Jumamosi ya Agosti 31, 2024 kuanzia saa 2:30 Asubuhi mpaka saa 11:00 jioni.

Hatua hii inatokana na ushauri na maoni ya wadau wa kodi, hivyo TRA inawakaribisha walipakodi wote kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali za kikodi.

Leave a Comment