×

Ni Historia Ruaha, Dkt. Samia Amwaga Miundombinu ya Utalii

Katika kile kinachoitwa misingi mitano ya utalii (Five As of Tourism) “A” mojawapo ni “attractions” hii tayari ipo Ruaha kwani wanyama wako lukuki lakini Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza miradi ya kimageuzi inayotekeleza “A” nyingine za “Access” “Ammenities” “Accomodations” “Activities” na “Affordability” katika Hifadhi ya Ruaha.

Katika kuufungua utalii wa Kusini mwa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaweka historia ya kujenga miundombinu lukuki ikiwemo maeneo ya malazi kwa wageni na wanafunzi, uwanja wa ndege wa kisasa wa kilomita 1.8, vituo vya utafiti na zana mbalimbali za kisasa za ujenzi maduka, maktaba na maeneo ya kubarizi.

“Hapa leo tumefarijika, tumeona kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Mradi wa Regrow chini ya usimamizi mzuri wa Wizara ya Maliasili na Utalii,” anasema Mhe. Timotheo Mnzava(Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.

Maboresho hayo yanamgusa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana(Mb) anayemshukuru Rais Dkt. Samia kwa uamuzi na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali na Benki ya Dunia kupitia mradi wa Regrow.

CCM WATOA TAMKO KIFO CHA ALI KIBAO wa CHADEMA ALIYETEKWA na KUUAWA – ”UBINADAMU SIASA PEMBENI”…

Leave a Comment