
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Makamu wake, Tundu Lissu wametaka matukio ya utekaji na mauaji yachunguze na chombo cha kimataifa walichokitaja kwa jina la Scotland Yard walipokuwa wakizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Septemba 11, 2024 katika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
Kufuatia matamko yao, chombo hicho kimezungua gumzo wengi wakijiuliza ni akina nani hasa?
Ni jukumu letu GLOBAL TV kukujuza hao Scotland Yard ni nani na kwa nini waitwe kuja nchini Tanzania kuchunguza matukio hayo?
Iko hivi; Scotland Yard ni Idara ya Uchunguzi ya Polisi iliyopo jijini London nchini Uingereza ambayo inahusika na kulinda raia na kuhakikishia usalama wao ikiwemo kufanya uchuguzi, udhibiti wa matukio ya uhalifu sugu wa mitaani na matukio ya ugaidi ya kimataifa.

Awali, Makao Makuu ya Scotland Yard yalikuwa katika Mji wa Metropolitan jijini London nchini Uingereza.
Mara nyingi idara hiyo ya Polisi hufahamika kama Scotland Yard kutokana na chimbuko la jina la Ofisi za awali.
Kwa hivi sasa ofisi za Polisi wa Scotland Yard zipo katika Mji wa Westminster; mji wenye hadhi kati ya miji iliyopo jijini London.
Scotland Yard inafanya kazi kwa njia nyingi za kitaalam za kiuchunguzi ikiwemo FORENSIKI yaani uchunguzi wa kipolisi kwa kutumia mbinu za kisayansi na teknolojia ili kuchunguza na kutatua kesi za uhalifu.
Forensiki inahusisha uchambuzi wa ushahidi wa kimwili au wa kidijitali ili kusaidia katika kubaini ukweli wa matukio au kutambua wahusika wa uhalifu.
Hii inaweza kujumuisha mambo kama vile Uchambuzi wa Nyenzo; yaani kutumia mbinu za kisayansi kama vile DNA, vichafuzi vya kemikali au uchambuzi wa alama za vidole ili kupata taarifa muhimu kutoka kwa nyenzo zilizopatikana kwenye eneo la tukio.
Pia wanafanya Uchambuzi wa Digital; yaani Kuchunguza vifaa vya elektroniki kama vile kompyuta, simu za mkononi na vifaa vingine vya kidijitali ili kupata taarifa au ushahidi wa kidijitali unaoweza kusaidia katika kesi.
Pia wanafanya Uchambuzi wa Alama za Mikono na Mguu; yaani Kutambua alama za vidole, alama za miguu au alama nyingine za kimwili ili kuona kama zinaweza kuhusishwa na wahalifu au watu wengine.
Wanafanya Uchambuzi wa Mahali pa uhalifu; yaani Kuchunguza mazingira na vitu vilivyokuwepo kwenye eneo la tukio ili kuelewa jinsi tukio lilivyotokea na kutoa picha ya wazi zaidi kuhusu matukio ya tukio hilo.
Mbali na hilo wanafanya Uchambuzi wa Kielelezo; yaani Kuchunguza picha, video na nyaraka za eneo la tukio ili kupata picha sahihi ya tukio.
Mchakato huu unahitaji ujuzi wa kitaaluma, umakini na teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha kuwa ushahidi unaopatikana unakubalika mahakamani na unaweza kusaidia katika kuhakikisha haki inatendeka.
Baada ya kupata mwanga huo, sasa yafuatayo ni baadhi ya majukumu makuu na jinsi wanavyofanya kazi;
Mosi; wanafanya Uchunguzi wa Uhalifu;
Scotland Yard ina vitengo maalum vinavyoshughulikia uhalifu mkubwa wa kimataifa kama vile mauaji, ulaghai na ugaidi.
Scotland Yard wanatumia mbinu za kisasa za uchunguzi, teknolojia ya juu na ushirikiano na mashirika mengine ya usalama na kijasusi duniani kama CIA, FBI, M16, MOSSAD, ISI GRU, SCORPION na mengine.
Pili; wanafanya Ulinzi wa Umma; Scotland Yard wanahakikisha usalama wa umma kwa kudhibiti matukio ya umma, kudhibiti uhalifu wa mitaani na kutoa msaada kwa jamii.
Wanaweza kuunda mipango ya usalama kwa matukio makubwa au maeneo yenye hatari.
Tatu; wanazuia Uhalifu;
Scotland Yard wanatekeleza mikakati ya kuzuia uhalifu kupitia ushirikiano na jamii, elimu ya umma na uchunguzi wa mapema.
Hii inaweza kujumuisha kuanzisha miradi ya kijamii na kuanzisha uhusiano mzuri na wananchi.
Nne; wanashughulikia Maelezo ya Kiwakili:
Kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kisheria ya kimataifa, wanachambua na kutumia taarifa za kiintelligensia ili kubaini vitisho vya usalama na kupanga hatua za kuzuia.