
Crispin Ngushi amefunga bao lake la pili la msimu akiingia kambani mara moja wakati Mashujaa Fc ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Wanamangush, Coastal Union katika dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam.
Nyota huyo wa zamani wa Yanga Sc alifunga bao lake la kwanza dhidi ya Dodoma Jiji Fc kwenye mchezo wa raundi ya kwanza kabla ya kuandika bao lake la pili la msimu dhidi ya Wagosi wa Kaya.
FT: Coastal Union 0 – 1 Mashujaa FC
⚽ Ngushi 14’
Mashujaa Fc wamekwea mpaka nafasi ya pili wakiishusha Simba Sc kwenda nafasi ya tatu huku huku Coastal Union ikisalia nafasi ya 13 baada ya kukusanya alama moja tu kwenye michezo miwili.
