
Mkutano wa Red Cross na Crescent Network ni Mkutano unaohusisha Nchi wananchama wa Red Cross ukanda wa mashariki na bahari ya Hindi amabapo nchi 16 zimeshiriki mkutano huo uliofanyika leo tarehe 18 septemba katika Hotel ya Mount Meru jijini Arusha, Tanzania Mkutano huo ambao umehudhuriwa na viongozi wakuu wa Nchi wanachama wa Red Cross yaan Marais na Makatibu Wakuu
Akitoa salaam mwenyeji wa Mkutano huo rais wa Tanzania Red Cross Society Mh. David M Kihenzile mbali na kuwakaribisha ametoa muelekeeo wa TRCS jinsi inavyoisadia serikali katika kupambana na majanga mbalimbali na kutoa shukrani zake kwa wadau wote ambao wamekuwa wanasaidia Tanzania Red Cross Society vilevile ameelezea ushirikiano wa serikali ya Tanzania na TRCS katika kusaidia jamii ya kitanzania.
Mheshimiwa David Kihenzikle pia ametumia nafasi hiyo kutangaza utalii na kuonesha uwepo wa Royal Tour kampen,i kampeni ambayo ilizinduliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivyo basi wao kama wenyeji wanaunga mkono kampeni hiyo na baada ya M kutano huu washiriki wote wataelekea katika hifadhi ya Taifa Ngorongoro kwaajili ya kufanya utalii nakujionea vivutio mbalimbali.
Vilevile mh. David Kihenzile ameelezea umuhimu wa Tanzania katika nchi hizo jinsi ambavyo itaweza kuwaunganisha wanachama hao kwani serikali ya Tanzania inaendelea kujenga miundo mbinu imara kama vile ambayo itawaunganisha katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo
Akimkaribisha Mgeni Rasmi wa Mkutano huo ambaye ni Makam wa rais wa IFRC Ukanda wa Afrika Bolaji Akpan Anani ametumia nafasi hiyo kuomba wanachama na viongozi wa Tanzania Red Cross Society wapate nafasi ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya IFRC ambapo kwa wakati huu tunao wagombea wawili CPA T. Japhet Shirima na George Nangale .
Akifungua mkutano huo Mgeni Rasmi Makam wa rais wa IFRC ukanda wa Afrika amesema tutakuwa hapakwa siku chache ambazo zitakuwa nzuri na za thamani katika National Society tunazoziongoza hivyo basi ninaomba tushiriki kwa ukamilifu ili kwapamoja tuweze kubainisha na kuainisha vipaumbele vyetu kwaajili ya kujenga National Society zenye nguvu.
Mkutano huo pia umehudhuriwa Katibu Mkuu IFRC Ukanda wa Afrika ndg. Mohammed Mukhier pamoja na wawakilishi kutoka ICRC pamoja na wajumbe wa NEC wa Tanzania Red Cross Society.