×

WCF Watoa Elimu ya Fidia Kwa Waajiri

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi pamoja na masuala ya msingi ya kulinda usalama na afya mahali pa kazi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma  mjini Iringa wakati akifungua kikao kazi kilichoandaliwa na mfuko huo kwa Maafisa Tawala, Maafisa Utumishi na Maafisa Usalama na Afya mahali pa kazi kutoka mikoa ya Iringa na Njombe, Songwe, Dodoma, Arusha na Dar es Salaam.

Mduma ameongeza kuwa pamoja na jukumu la msingi la kutoa fidi kwa wafanyakazi wanaoumia au kuugua kutokana na kazi, kulipa wategemezi wa mfanyakazi atakayefariki kutokana na kazi, Kukusanya michango pia WCF ina jukumu la kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo katika maeneo ya kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Tathmini WCF Dkt. Abdulsalaam Omar alisema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki kuhusu namna ya kutoa taarifa kwa wakati kuhusu ajali na magonjwa yanayotokana na kazi, vilevile namna ya kubaini viashiria vya hatari katika sehemu za kazi.

Katika kikao kazi hicho mada mbalimbali zinawasilishwa ikiwa ni pamoja na taratibu za uwasilishaji madai kwa njia ya mtandao, haki na wajibu wa mwajiri na mwajiriwa katika kuwezesha WCF kushughulikia kwa ufanisi madai ya fidia kwa wafanyakazi na kanuni muhimu za kuzingatia ili kulinda na kudumisha usalama na afya mahali pa kazi.

 

Leave a Comment