
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Ndugu Nenelwa Joyce Mwihambi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Ndugu Baraka Ildephonce Leonard kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Septemba, 2024.


