×

Ni Kidigitali Zaidi! Tigo na TRC Warahisisha Ununuzi wa Tiketi za SGR

Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha.

Kampuni ya Mawasilino ya Tigo imezindua mfumo mpya wa ulipaji wa tiketi za Reli ya Kisasa (SGR) kupitia huduma zake za kidijitali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha, ameelezea kuwa mfumo huu unalenga kurahisisha mchakato wa ununuzi wa tiketi ambapo Abiria sasa wataweza kukata na kulipia tiketi zao kwa urahisi kwa kutumia simu zao za mkononi, huku wakiepuka foleni ndefu.
“Ushirikiano wetu na TRC unaonesha dhamira yetu ya kuboresha huduma za usafiri na urahisi kwa wateja,” alisema Pesha. “Tigo Pesa inajitahidi kuwa mfumo wa kifedha ulio jumuishi kwa Watanzania wote.”
Pesha pia amesisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa kifedha, akionyesha jinsi huduma za Tigo Pesa zinavyoweza kuboresha maisha ya watu binafsi na jamii kwa ujumla. Mfumo wa ulipaji wa tiketi unaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri, huku ukisaidia kuimarisha uchumi wa kidijitali nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.                                                                                          Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, ametoa pongezi kwa Tigo Pesa kwa kuleta ubunifu huu, akisema ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya umma ni muhimu katika kuleta maendeleo ya kitaifa.
Tigo Pesa inatarajia kuendelea kuimarisha huduma zake, huku ikihakikisha kuwa kila Mtanzania anapata fursa ya kushiriki katika uchumi wa kidijitali.
Picha ya pamoja

Leave a Comment